Sale!

Mikondo ya Kiswahili: Siasa, Jamii na Utandawazi

900.00KSh

Ni kitabu chenye mawazo ya kina na maki kuhusu maenezi na maendeleo ya Kiswahili.

Category:

Description

Ni kitabu chenye mawazo ya kina na maki kuhusu maenezi na maendeleo ya Kiswahili. Kitabu hiki kina sehemu mbili muhimu. Sehemu ya Kwanza inajishughulisha na maendeleo na mabadiliko ya kiisimu ya lugha ya Kiswahili na changamoto zinazokikumba. Mathalan,licha ya kuwa ukoloni ulisaidia kukiendeleza Kiswahili kupitia tafsiri na juhudi za usanifishaji, pia ulikiweka daraja ya chini kikilinganishwa na Kiingereza kwa njia ambayo haikukipa nafasi ya kutosha ya kukua na kupanuka kimsamiati. Kuna hoja kuhusu nafasi ya tafsiri katika ukuzaji wa Kiswahili na namna urithi wa Kiingereza unavyoathiri utamaduni wa kisheria na wa kikatiba wa nchi za Afrika Mashariki. Waandishi wanasisitiza umuhimu wa utumiaji wa Kiswahili katika sheria, katiba, mahakama na bunge katika kujenga utamaduni wa kikatiba na kisheria miongoni mwa wananchi wa kawaida. Sehemu ya pili inahusu nafasi na umuhimu wa Kiswahili katika enzi ya utandawazi. Ni kitabu muhimu sana kwa yeyote anayetaka kujua namna lugha hii ya Kiafrika inavyojitanua na kukubalika katika jamii mbalimbali.