KIDAISO SARUFI NA MSAMIATI

500.00KSh

Kitabu hiki kinafafanua Sarufi na Msamiati wa Kidadiso – lugha inayozungumzwa katika maeneo ya makoa wa Tanga Tanzania. Wadaiso ni jamii ndogo sana na wanajulikana na kujitambulisha kama wasegeju wa milimani.

Category:

Description

Kitabu hiki kinafafanua Sarufi na Msamiati wa Kidadiso – lugha inayozungumzwa katika maeneo ya makoa wa Tanga Tanzania. Wadaiso ni jamii ndogo sana na wanajulikana na kujitambulisha kama wasegeju wa milimani. Wanaaminika kuwa waliotoka katika eneo la kaunti ya kitui, kenya, ambapo lahaja ya Kiikamba Ijulikanayo kama kithaisu inazungumzwa. Katikati ya karne ya 16, kundi lao moja lilianza safari kuelekea mashariki.

 

Baadhiyao walivuka mto Tana na kuelekea malindi na Mombasa. Kwa uhoari wao wa vita  wakamsaidia mtemi mmoja wa Wadigo kuwashinda adaui zake; wakaweka makazi pamoja na Wadigo hawa na kuoa wake wa Kidigo. Mama hawa wa Kidigo wakawafunza watoto wao kuzungumza Kidigo. Matokeo yake ni kwamba Wadaiso hawa walipoteza lugha yao na kuzungumza lahaja fulani ya Kidigp, ikijulikana kama Kisegeju.